Balaa! Jux awajibu wanaodhani uhusiano wake na Vanessa Mdee umekwisha

Image: Jux-na-Vanessa-Mdee

Kumekuwa na uvumi mitandaoni kuwa Vanessa Mdee na Jux Juma wameachana baada ya Vmoney kuonekana akiwa na wanaume tofauti kwenye picha ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni.

Hata hivyo Jux amefunguka kuhusu maneno haya na kusema kuwa yeye anamuamini mpenzi wake kwani hata picha hizi zikichukuliwa yeye huwa akifanya kazi na hana tatizo na hilo.

download latest music    

Aliendelea kwa kusema pia yeye kuna wakati yeye hupiga picha na wanawake ambao anafanya kazi (project) na wao na hii haimanishi kuwa anatoka na wao. Jux alisema,

“Si kweli mimi nilimind, sababu kama kupiga picha za namna hizo Vanessa anapiga na watu wengi sana picha za namna ile. Naomba nirudi nyuma kusema hili tena wasichana kwenye tasnia yetu sisi wavulana ndiyo tunatakiwa kuwasupport sana kwa sababu wapo wachache.”

Aliongeza kwa kusema,

Muimbaji huyo ameongeza, “Mimi hata nikipiga picha na wanawake 10 hapa, watu watajua tu Jux anafanya video ila Vanessa akipiga picha hizo watu watasema huyu mwanamke mhuni.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua