Banana Zorro Afunguka Baada Ya Kuonekana Amevaa Msalaba

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Banana Zahir Zorrro amefunguka baada ya kuonekana akiwa amevaa msalaba wenye picha ya Yesu Kwenye shoo.

Banana Zorro amezua gumzo usiku mnene ukumbini baada ya kuonekana akiwa ametinga msalaba shingoni wenye sanamu ya Yesu Kristo msalabani huku ikifahamika kuwa ni Muislam.

download latest music    

Jambo hiko liliibua maswali kwa mashabiki zake ambao walitinga Kwenye shoo yake iliyofanyika Ukumbi wa Legend Park, Namanga jijini Dar es Salaam.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Banana Zorro alifunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni muislamu lakini aliamua kuvaaa rozari ile kwa sababu alizawadiwa na Marehemu mama yake:

Ni kweli mimi ni Muislamu  lakini huu msalaba ukweli ni wa Kikristo aliniachia marehemu mama yangu mzazi kwa kuwa alikuwa Mkristo“.

Banana ambaye ametokea kwenye familia ya wanamuziki kuanzia baba yake mpaka dada yake Maunda Zorro.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.