Banana Zorro- Wanaonichukulia Poa na Kudai Nimefulia Hawanijui Vizuri

Mwanamuziki wa Bongo fleva Banana Zorro aliyetamba miaka ya nyuma na ngoma kali kama Mama yangu, Rafiki, na Nzela ameibuka na kudai taarifa za kwamba amefulia sio kweli kabisa.

Banana ameibuka na kudai watu ambao wanasambaza habari kuwa yeye amefulia au hana mafanikio yoyote basi ni wazi kuwa watu hao hamjui vizuri.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Mwananchi Communication Limited, Banana amekataa taarifa za yeye kufulia kwa sababu tu hasikiki kama zamani:

Mtu anayeniambia mimi nimefulia au sijafanikiwa kimuziki, huyo atakuwa hanijui kiundani. Tena na hii lifahamike mimi ndio msanii wa kwanza kuwa na bendi yangu mwenyewe Tanzania na inafanya vizuri. Pia nimeajiri watu katika bendi yangu zaidi ya 20. Nafikiri hayo ni mafanikio makubwa sana kwangu“.

Banana aliyetokea kwenye familia ya kimuziki kwani Baba yake naye ni msanii Mzee Zahir Zorro Lakini pia dada yake ni msanii ambaye anajulikana kama Maunda Zorro.

Hivi sasa Banana anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaoitwa Mapenzi gani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.