Baraka The Prince Awasili Kwa Tundu Lissu

Yawezekana Baraka akawa ndio msanii wa kwanza kwenda kumtembelea Mh.Tundu Lissu tangu alipokutwa na matukio ya kupigwa risasi nyingi na kuwa mahututi kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili sasa.Jana,kuanza kwa  mwaka 2018 umeanza vizuri kwa Baraka na kwa Mh.Tundu Lissu pia baada ya wawili hao kupata bahati ya kuonana kwa mara ya kwanza tangu amepata majanga hayo.

Wasanii wengi walihaidi kwenda kumuona  mwanaharakati huyo akiwemo Wema Sepetu kipindi bado hajahama kutoka CHADEMA  kwenda CCM, lakini ndoto hiyo ilikatika baada ya mwanadada huyo kuhamia tena CCM.

download latest music    

Baraka The Prince ametua Nairobi na kwenda moja kwa moja mpaka hospitali aliyolalazwa Tundu Lissu kwa ajili ya kwenda kumjulia hali alkini bado haijajulikana kama Baraka The Prince aliamua kufunga safari tu mpaka Nairobi kwa ajili ya kumuona tu mwanasiasa huyo au alikuwa na shoo nchini humo au kuna kitu cha ziada zaidi ya hicho.

Hata hivyo mashabiki wa Baraka na wanachama na watu wengi wamefurahishwa na kitendo cha msanii huyo kujitokeza kama msanii wa kwanza kwenda kumuona mwanasiasa huyo kwa sababu tangu amepata matatizo wapo wasanii wengi wanaoimba harakati lakini hawajapata bahati ya kwenda kumuona huku baadhi ya mashabiki wakihisi kuwa huo ndio mwanzo wa msanii huyo kuanza kujiingiza katika siasa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.