Barakah The Prince Adai Kuchoshwa na Hujuma

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amerudi tena kwenye headlines za mitandao ya kijamii baada ya kudai kuwa amechoshwa na mtu anayemfanyia hujuma.

Mwezi uliopita Barakah alitengeneza headlines na kuzua balaa baada ya kuenda  kwenye vituo vya habari na kudai kuwa uongozi wake wa zamani ukiongozwa na Ali Kiba na meneja wake anauejulikana kama Seven wanamfanyia hujuma ili nyimbo yake mpya isifanye vizuri.

download latest music    

Barakah alijitoa chini ya uongozi wa Rockstar 4000 kwa kile alichodai kuwa walimchelewesha kutoa kazi zake katika wakati husika. Lakini  baada ya kuondoka huko alianza kuwatuhumu Alikiba na Seven kwa kumuhujumu na kudai wanatumia njia mbali mbali ili kizui nyimbo yake ya ‘sometimes’ isichezwe ikiwemo kiharibu utaratibu mzima wa akaunti yake ya Youtube ili asipate mashabiki wa kuangalia nyimbo yake.

Kutokana na hayo Barakah amefunguka na kudai kuwa amechoshwa na hujuma hiyo anayofanyiwa kwenye mtandao wa youtube na kuamua kutangaza dau la milioni tano kwa yeyote atakayeweza kumgundua mtu atakayeweza kumtambua mtu anayepunguza watazamaji wake kwenye mtandao wa Youtube.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio Barakah alizidi kufunguka yafuatayo:

Kwanza nishukuru mashabiki zangu mnaozidi kunipigania na kupoteza muda wenu kwa ajili ya kazi zangu lakini kuna mtu mmoja ambaye aliumbwa kwa ajili ya kurudisha nyuma hatua za watu kila siku views zinazidi kupungua sasa basi matangaza kumpa mtu dau la milioni 3 kwa yeyote atakayethibitisha na kutuletea huyo mtu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.