Barakah The Prince Adai Ali Kiba Anampotezea

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai Msanii mwenzake Ali Kiba amekuwa akimpotezea na kukataa kujibu meseji zake anazomtumia.

Sakata kwa Ali Kiba na Barakah The Prince lilianza mara baada ya Barakah kuamua kujitoa katika label ya Ali Kiba Ya Rockstar 4000 kwa madai ya kutosimamiwa vyema na kazi zake kuthaminiwa.

download latest music    

Lakini baada ya kutoka kwenye Label hiyo Barakah aliitupia tuhuma nzito na pia kumtuhumu Ali Kiba kwa kufanya kila njia kumharibia muziki wake ikiwemo kumfutia Chanel yake ya Youtube na kufuta nyimba anazotoa ili asifike mbali.

Tuhuma hizo hazijawahi kujibiwa na Ali Kiba lakini Barakah baadae alienda kuomba radhi kwa maneno hayo, Lakini sasa Barakah ameibuka na kudai amekuwa akijaribu kumtafuta Ali Kiba lakini meseji zake hazijibiwi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo,Barakah amefunguka haya kuhusu jitihada zake za kutaka kumtafuta Ali Kiba.

Nilishawahi kumtext nikamwambia brother kuna hichi na hichi na haya ni maisha na haya mambo ambayo yanayoendelea tuachane nayo tudeal na maisha mengine, mimi bado ni kijana nahitaji muongozo wao ili nifanikiwe”.

Barakah amefunguka na kusema pamoja na kumtumia meseji Ali Kiba meseji na kutojibu Lakini pia alimtumia meseji ya msamaha Seven Mosha, Kidboy na Mgagulah ambao wote hawakujibu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.