Barakah The Prince Akiri Tetesi Za Kufulia

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa tetesi zilizokuwa zinasambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa amefulia zilikuwa za kweli.

Baada ya kuondoka chini ya uongozi wa Rockstar 4000 Barakah aliamua kufanya kazi mwenyewe kwa kile alichodai kuwa chini ya uongozi ule alikuwa hapati mafanikio kwani alikuwa haruhusiwi kutoa nyimbo na hata kufanya shoo.

download latest music    

Barakah ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Sina’ ambao amekiri Kwenye wimbo huo kuwa kipindi hiko amekuwa hana pesa yaani amefulia vibaya mno na chanzo ameweka wazi kuwa ni kuwa chini ya uongozi uliomzuia kufanya shoo kwa mwaka mzima.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kwamba Barakah ameishiwa kabisa hana kitu yaani kafulia na kwenye mahojiano yake na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Barakah amefunguka haya zaidi:

’ Sina’ ni wimbo wangu ambao naweza kusema nimeurekodi wakati nikiwa katika situation mbaya sana kimaisha yaani kuna siku naamka naangalia king’amuzi kimeisha, Tv haiwaki naangalia ndani sina chochote na gari haina mafuta nikasema haya maisha gani haya.

Kama mtakumbuka mwaka jana sikufanya shoo kabisa kutokana na situation iliyotokea kwaiyo nilikuwa siruhusiwi kufanya shoo yoyote kwaiyo nilikuwepo tu kwaiyo huu wimbo ‘Sina’ nimeuvaa uhusika kwa sababu nilikuwepo katika hiyo situation”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.