Baraza la Sanaa Tanzania yatoa kauli yake kuhusu picha za utupu za Ben Pol

Ben Pol alizua uzushi katika jukwaa zote baada ya picha zake za utupu kuibuka katika mitendao za kijamii siku chache zilizopita.

Msanii huyo alionekana akiwa uchi wa mnyama katika picha za kitaalamu alizopiga. Watu wengi walikerwa na picha hizo licha ya sehemu yake nyeti kutoonekana.

download latest music    
Moja ya picha ambazo Ben Pol aliweka kwenye mtendao wa kijamii

Baraza la Sanaa Tanzania – BASATA limetoa kauli yake kuhusu picha za Ben Pol. Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alilaani kitendo cha Ben Pol na kusema kwamba sanaa ya Tanzania bado haijafikia zama za kufanyika kitendo kama hicho.

“Kwa tamaduni zetu bado hatujafikia hapo ni wengine huko ambao wanaruhusu. Hiyo ni moja, pili ni kitendo ambacho baraza inakilaani lakini kwa utaratibu wa baraza kama baraza tutamtafuta Ben Pol tuweze kumsikia mwenyewe kwamba zile picha kweli amepost yeye au kuna kitu kingine kwa sababu teknolojia imekwenda mbali sana siku hizi kwahiyo tutamsikiliza anahusika vipi moja kwa moja. Lakini kimsingi kwa ujumla wake baraza inakilaani na tutaendelea kumtafuta Ben Pol kuzungumza naye kwa sababu ni haki yake kusikilizwa katika hilo.

“Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol,”alisema Godfrey Mngereza.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere