Barnaba Akiri Bado Anampenda Mama Steve

Msanii wa muziki wa siku nyingi Barnaba amefunguka na kuandika ujumbe mrefu huku akisema kuwa katika maisha yake yote hawezi kuacha kumpenda mama wa mtoto wake ambae ndie aliekuwa mpenzi wake kwa miaka 9 aliokaa nae tangu alipoanza muziki alipopambana na hata kufikia hapo alipo.

Barnaba anasema kuwa katika maisha kuna mapenzi na mapendo lakini aliyonayo kwa mama steve ni mapenzi ambayo anaamini kuwa hayaweiz kuisha hata kitokeee nini kamwe haweiz kuacha kumpenda mama huyo.

download latest music    

Barnaba anasema kuwa yeye na mama steve watabaki kuwa ndugu tu kwa sababu ya mtoto wao anaewaunganisha na hata siku moja haweiz kumchukia mama wa mtoto wake, lakini pia barnaba amezungumzia swala la mpenzi wake wa sasa kuwa mjamaizto kwa kusema kuwa watoto wamekuwa baraka katika maisha ya kila siku hivyo hata yeye  hawezi kuliongelea hilo.

Ikumbukwe kuwa zuu ambae ni mama steve alianza kuonekana akiwa na mwanaume mwingine na ndipo ilipojulikana kuwa wawili hao wameachana pamoja na kwamba mara nyingi barnaba amekuwa akitunga nyimbo zinazoonyesha kuumizwa sana na kuachwa na Mama Steve.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.