Barnaba Amedai Yeye Sio Wa Kawaida Kawaida Ameajiri Bodyguard

Msanii wa Bongo fleva mkali wa voko toka longtime kitambo Barnaba Classic amefunguka nini hasa kilichomsukuma kukodi bodyguard ambaye anatembea naye kila sehemu.

Siku za hivi karibuni Barnaba amekuwa akionekana sehemu mbali mbali kama kwenye matamasha na club kwenye shoo akiwa na mlinzi wake binafsi almaarufu kwa jina la bodyguard.

download latest music    

Kwa Bongo msanii pekee ambaye Ana kawaida ya kuwa na bodyguard ni Diamond Platnumz ambaye mara kwa mara amekuwa akionekana na bodyguard wake ambaye hata husafiri naye kwenda sehemu mbali mbali.

Barnaba alikuwa mmoja kati ya wasanii wachache waliohudhuria tamasha liliondaliwa na East Africa TV la 5 select ambapo alienda kwenye tamasha hilo akiwa ameandamana na body guard wake na alifunguka sababu za kutafuta bodyguard kwa sasa:

Mimi kuwa na bodyguard ni ku-add  value kuongeza thamani kwenye kile ninachokifanya lakini pia nikatika kuhakikisjha usalama wangu binafsi na maisha yangu hasa kwenye kazi zangu of course sisi ni watu wa watu tunafanya kazi kwa ajili ya watu lakini kuna watu wanakujia sio kwa nia nzuri lakini hii pia nichachu ya kuonyesha thamani ya Barnaba sio mtu wa kawaida kumfikia kirahisi rahisi Lakini pia huyu mlinzi ananisaidia kulinda usalama wangu binafsi kwani mimi ni staa”.

Lakini pia Barnaba ameelezea vitisho anavyopokea kila siku vimemsukuma yeye kutafuta mtu wa kuangalia usalama wake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.