BASATA Wajenge Urafiki na Wasanii-Ben Pol

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amewafungukia BAraza la sanaa Tanzania (BASATA) na kuwataka kujenge mazingira rafiki na wasanii.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Ben Pol ameweka wazi kuwa ni muhimu kwa BASATA kutengeneza urafiki na ukaribu na wasanii ili kuondoa ile dhana ya kuhofia pale wanaposikia wanaitwa BASATA.

download latest music    

Tangu Mwanzoni watu walikuwa wanaitwa BASATA kwa matatizo lakini ingekuwa kuna Ukaribu fulani yaani wangeanza hadi kuita wasanii kwa ajili ya mambo mazuri kama kupongeza wasanii kwa ajili ya kushinda tuzo ingekuwa vizuri.

Sasa hivi imekaa Kwenye akili za watu wengi kama ukiitwa BASATA basi ujue ni msala lakini wakijenga mazingira rafiki na wasanii basi kutakuwa na matokeo chanya katika sanaa na uhusia Mzuri”.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na mvutano mkubwa baina ya wasanii na BASATA hasa linapokuja suala la sheria mpya na maadili za nyimbo wanazotoa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.