Batuli Afunguka Kuwa Wanaorusha Picha za Utupu Mtandaoni Sio Wasanii

Muigizaji na msanii wa Bongo movie Batuli the actress amefunguka na kudai kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni wasanii wanaokaa uchi Mara nyingi wanakuwa sio wasanii bali watu waliojipatia umaarufu kwa njia hiyo ya kukaa uchi mtandaoni.

Siku chache zilizopita Naibu waziri wa Habari Juliana Shonza aliuwasha moto baada ya kukemea wasanii kuvaa mavazi ya nusu uchi mtandaoni ambapo alimtaja msanii kama Pretty Kind ambaye alijulikana kwa kuvaa uchi kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliishia kufungiwa kufanya sanaa yoyote kwa muda wa miezi sita.

download latest music    

Lakini msanii mwingine aliyeingia kwenye maji ya moto ni Gigy Money ambapo alitakiwa kuripoti Basata kwa mavazi yake ya nusu uchi lakini pia wimbo wake wa Nampa papa uliosemekana kukosa maadili.

Batuli amefunguka kwenye ukurasa wake Instagram na kudai kuwa tasnia ya filamu na muziki inachafuliwa na watu wanaojifanya kuwa wao ni wasanii wakati sio wasanii.

Asilimia kubwa ya wanaotupia picha chafu kwenye mitandao ya kijamii hawapo kwenye makundi haya mawili muziki na filamu umaarufu wao wameupata kwa kupiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii na watanzania wasio kuwa na maadili kuwapokea kwa shangwe #Sanaa ipewe heshima yake”.

Wasanii wengi kama Gigy Money na Pretty Kind walianzia umaarufu wao kwa kurusha picha za utupu mtandaoni na baada walijiingiza kwenye sanaa ya muziki.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.