Beka Athibitisha , Anakaribia Kuitwa Baba.

Mwanamuziki Beka Flavour amethibitisha kuwa hivi karibuni ataitwa baba kutokana na ukweli kuwa mpenzi wake  wa siku nyingi kwa sasa ni mjamzito.akiongea kwa kujiamini, beka anasema kuwa huyo ndio atakuwa mtoto wake wa kwanza na kwamba katika kundi lao lilivunjika ni yeye pekee ndio alikuwa hana mtoto hata mmoja.

Beka ambae hivi karibuni alitoa wimbo mpya anasema kuwa ametoa wimbo huo ili uwe maalum kwa mwanamke wake huyo ambae alianza nae mapenzi kabla hajaanza muziki na mpaka sasa huku wakipitia mambo mengi hapo katikati ikiwa ni pamoja na ugumu wa maisha lakini hakukata tamaa zaidi ya kuwa anampa moyo na kumfarijikwa kila hali.

download latest music    

Akitoa sababu ya kuchelewa kupata mtoto, Beka anasema kuwa kwa jinsi mapenzi aliyokuwa nayo mwanadada huyo aliona kuwa ni bora kwanza akae vizuri kifedha ndipo aone jinsi ya kuongeza mtoto ili asije aka mtesa binti wa watu alikaa nae katika shida na raha zote.

Nimejikuta nimeshindwa kujizuia kupost hii picha na hivi karibuni nitatwa baba,furaha niliyonayo haipimiki kwani huyo atakuwa mtoto wangu wa kwanza.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.