Beka Flavor aeleza baadhi ya changamoto alizopitia Yamoto Band

Beka Flavor amekuwa akijishughulisha na projects mbalimbali baada ya kutoka Yamoto Band. Kama Aslay ambaye walikuwa wakipiga kazi za mkubwa na wanawe Pamoja, pia anafanya nyimbo zake akiwa Solo.

Hii inakuja baada ya wasanii hao kuamua kuwa wangefaidika zaidi ikiwa wangefanya projects zao wakiwa Kama solo artists. Hata hivyo Beka Flavor hivi karibuni amefunguka kudai kuwa kuimba Kama bendi ilikuwa na Changamoto zake.

download latest music    

Akizungumza na kipindi cha Dj Show cha Radio One, Beka alisema…

“Vitu vingi vilikuwa vinanizuia, kwanza nilikuwa si-enjoy kwa sababu nilikuwa naimba verse fupi, mwenywe nilikuwa natamani niimbe verse ndefu lakini wenzio wataimba wapi, hicho ni kitu cha kwanza kilikuwa kinanibana,”

Aliongeza kusema,

“Kuna vitu vingi vimefunguka kupitia mimi mwenyewe, kwanza ilikuwa mtu akinihitaji ni lazima apitie kwa mtu mwingine na mwingine, au kuna kitu kingine ambacho mimi napenda kufanya zaidi ila uongozi unakuta unabana lakini sasa hivi vile navyopenda kuvifanya nafanya na uongozi upo.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua