Beka Flavour Afungukia Tetesi Za Kufunga Ndoa Kimya Kimya na Mpenzi Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Siwezi’ Beka Flavor amefungukia tetesi zinazosambaa Kwenye social media kuwa amefunga ndoa na mpenzi wake.

Siku za nyuma Beka Flavor alishawahi kusikika akisema kuwa hawezi kumuanika mpenzi wake Kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu hajatoa mahari kwao.

download latest music    

Lakini baadae alianza kumuanika mitandaoni na hata kuonekana ni mjamzito na baadae ilisemekana wawili hao wanaishi nyumba moja na Habari za chini ya kapeti zikadai wawili hao wamefunguka ndoa kwani Msichana huyo alibadilisha dini.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Beka Flavor amefunguka na kusema hawezi kuanika kila kitu Kwenye mitandao ya kijamii

Kwa sasa naishi na mpenzi wangu geto, lakini mimi ni mtoto wa kiislamu siwezi nikakurupuka kuishi na mtoto wa watu ingawa siwezi kuanika Maisha Yangu binafsi Kwenye mitandao ya kijamii”.

Lakini pia Beka Flavor amethibitisha ameshamvhumbi mpenzi wake huyo na hivi sasa muda wowote wanategemea kuzaa mtoto wao wa kwanza.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.