Beka Flavour Asema Hayuko Tayari Kurudi Ya Moto Band

Moja wa wasanii walikuwa wakiunda kundi la Ya Moto Band amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye hayuko tayari kabisa kurudi Ya Moto Band hata kama kundi hilo litarudi kwa sababu kila mtu kwa sasa anasimama mwenyewe na anajua kuwa kundi ilo lilishakuffa.

Beka alisema kuwa wakati wanaondoka katika kundi ilo kipindi linavunjika waliondoka bila kuwa na ela yoyote , ilhali kipindi wanafanya kazi walikuwa wakipewa ela kidogo sana kwa ajili ya matumizi binafsi huku wakiwa wamependekeza kuwa ela zinazopatikana kutokana na kazi yao zifanyiwe matumizi kama vile kujenga nyumba lakini waliondoka bila ela yoyote,

download latest music    

“Mimi saivi uniambie nitoke kwenye uongozi wangu mpya afu nirudi Ya Moto sidhani kama itawezekana kabisa,unajua kuwa watu hawajui tu kuwa lile kundi lilishakufaga siku nyingi tu, kwa sababu saivi kila msanii yupo katika uongozi wake,sidhani kama kuna mtu atakubali atoke huko alipo kwenye uongozi wake aje tena kurudi katika kundi la Ya Moto Band” Alifunguka

Msanii huyo ambae saivi anafanya vizuri na kibao chake cha sikinai, anasema kuwa kwake yeye ni furaha anapoona wasanii aliotoka nao kundi moja wanapofanya vizuri, akiongelea upande wa Aslay anasema kuwa anafurha kuona aslay sasaa hivi amekuwa msanii anaeongelewa kila sehemu kutokana na kazi zake nzuri.

“Mimi nazidi kumuombea mwenzangu, maana amekuwa ni mmoja wa wasanii ambao wanazungumziwa sana  kutokana na kazi zake nzuri anazofanya,lakini napenda pia kuwaambia watanzania kuwa wasanii  ambao tulikuwa tukiunda kundi hili la Ya Moto Band Mungu alitupa vipaji vyetu maarum, kuna kitu aliweka ndani yetu , kwaio sio muda mrefu  mtakuja kuona haya ninayoyasema kwani kila mmoja wetu  ana upekee wake kwenye kazi. alisema Beka Flavour.

Kundi la Ya Moto Band lilikuwa ni moja ya makundi yalikuwa yakifanya vizuri nchini Tanzania , lakini baadae lilikuja kuvunjika huku hakuna uongozi uliotaka kuweka wazi sababu za kuvunjika kwa kundi ilo.Hata hivyo baadhi ya wasanii wa kundi ilo wameanza kuonyesha juhudi zao nje ya kundi akiwemo Aslay.

Wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Ya Moto Band

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.