Bekaflavour Agoma Kuwa Chanzo cha Kuvunjika kwa Ya Moto

Msanii Beka flavour amefunguka na kusema kuwa hata siku moja hataki kupokea lawama anazorushiwa kuwa yeye ni moja kati ya sababu ya kundi lao la Ya Moto kuvunjika miaka ya nyuma na kusababisha kila mtu kufuata ustaarabu wake.

Beka anasema kuwa mashabiki inatakiwakufika sehemu na kukubaliana na matokeo na  kuwa kila kitu kina muda wake lakini sio kurusha lawama na kumtafuta mchawi nani katika hilo, Hata hivyo swala la kuvunjika kwa kundilimeweza kusababisha watu kujiongeza na kupambana zaidi.

download latest music    

Beka anasema kuwa kwa kumbukumbu yake anajua kabisa kuwa hakuwahi kugombana na mtu katika lile kundi zaidi ya mmoja tu na haikusababisha kugombana sana kwa sababu walikuja wakakaa sawa.

Utakumbuka kuwa wasanii hawa walikuwa wakifanya kazi pamoja katika kundi moja lakini baadae kila mmoja alikwenda na njia yake baada ya kundi hilokushindwa kuendelea.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.