Ben Pol aeleza kwanini hana majuto kuhusu picha zake za utupu

Ben Pol alizua utata picha zake za utupu zilipotokea kabla ya yeye kuwachia wimbo wake ‘Tatu’. Staa huyo alionekana akiwa uchi wa mnyama kama ameketi kwa kiti huku mikono zake zimefungwa na uso wake kufunikwa.

Ben Pol alisema picha zake za utupu ziko na mchango mkubwa sana kwa maisha yake, alieleza kuwa picha hizo ni sehemu ya vitu ambayo amepitia ili vimjenge katika maisha yake.

download latest music    

“Hamna majuto, ni mafundisho tu…hamna majuto…hakuna majuto sehemu yoyote ila kila siku tunajifunza vitu vipya maana mimi akili yangu nilivyo iset napenda kupokea vitu vipya kujifunza kila siku. Sijawai kuwa comfortable ata uimbaji wangu mimi mbaka leo naskiliza mbinu mpya za kuimba, mbaka leo nafanya mazoezi, mbaka leo nagundua muziki mpya. Kwa hivyo kila kitu ni kujifunza tu kinavyoenda unaimprove, saa ingine unakutana na reaction mbaya inakujenga unakua imara kwa hivyo ndivyo hivyo inavyokua,” Ben Pol aliambia Bongo 5 alipoulizwa kama yupo na majuto kuhusu picha zake za utupu.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere