Ben Pol Ajutia Uamuzi Wake Wa Kutoa Albamu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefungukia na kudai anajutia uamuzi wake wa kutoa Albamu.

Siku za hivi karibuni wasanii wengi wamerudi kwenye trend ya kutoa Albamu baada ya kukomea kwenye kutoa single kwa muda mrefu hatimaye Siku za hivi karibuni wasanii kadhaa wamejaribu kuingia kwenye upande wa kutoa albamu.

download latest music    

Baadhi ya wasanii ambao wametoa albamu ni pamoja na Diamond Platnumz, Chinbees, Vanessa Mdee, Ben Pol lakini tofauti na wasanii wengine ambao wametoa Albamu, Ben Pol amejutia uamuzi huo wa kutoa Albamu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv, Ben Pol amefunguka na kusema amejuta kufika albamu yake ya The Best Of Ben Pol kwani faida aliyopata Kwenye mauzo ya albamu nzima ni sawa na shoo moja ambayo huwa anafanya:

Bado ni changamoto kusema kweli kwa sababu tukiongelea albamu yangu ya zamani ya 2011 mauzo yake yaliyonifikia mimi ni sawa na mauzo ya shoo yangu moja kwaiyo unaweza ukaona tatizo Lakini pia zamani tatizo lilikuwa kwetu wasanii tulikuwa hatutoi albamu lakini sahivi albamu tunatoa mashabiki hawanunui albamu zetu”.

Lakini pia Ben Pol amewataka mashabiki waache kuongea kuhusu wasanii kutoa Albamu badala yake waanze kununua kazi za wasanii ili wawape sapoti ili wao kuepuka kukata tamaa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.