Ben Pol apata dili kubwa baada ya picha zake za Uchi

Msanii wa Tanzania Ben Pol aliwaacha wengi kama wameduwaa baada ya kuachia picha zake huku akionekana uchi. Kama kawaida mashabiki walimponda na wengi kumkashif kwa kuachia picha kama zile mitandaoni ya kijamii.

Hata hivyo msanii huyo sasa hivi amepata dili na kampuni ya mafuta ambayo imempa jukumu la balozi. Ben Pol alifunguka kuhusu dili hiyo alisema,

download latest music    

“Hapa sasa hivi tunaongea kuhusu majukumu yangu kama balozi, nione nina show ngapi katika hiyo event na mambo ya maslai inakuaje, anione matangazo ya runinga na mabango na nijue amount ya kazi yote ilivyo ni kiasi gani ninaweza kunufaika.Tukifikia muhafaka watu wataniona kwenye mabango, nimekoleza mafuta nimeweka na logo za hiyo kampuni,” 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua