Ben Pol Asema Hawezi Kutoka Na Wema Sepetu Wala Jokate

Msanii ambae kwa muda sasa amekuwa akifanya vizuri katika  musiki wa Bongo Fleva, na kupokea  shangwe la kutoka kila anapopandwa majukwaani tena hasa kwa kipindi hiki cha tamasha kubwa la muziki la Fiesta likiendelea Ben  Pol ameonekana kukubalika sana na mashabiki wake. Hivi karibuni mashabiki zake wamekuwa wakimwita ‘king of Rnb’  na kumfanya yeye kuanza kutembea na fimbo ambayo yeye mwenyewe anasema ni ishara ya ufalme wake. Ben Pol amefunguka na kusema kuwa kwa yeye hawezi kabisa kutoka katika uhusiano wa mapenzi na wema sepetu wala jokate mwegelo.

Ben Pol ambae kwa sasa amekuwa na scandal ya kuwa na mahusiano ya kumapenzi na msanii wa maigizo ya uchekeshaji anaejulikana kama Ebitoke.Katika tetesi izo  Ben Pol mwenyewe alikanusha na kusema yupo na Ebitoke  kwa sababu anataka kumsaidia katika kazi zake za sana na si kitu kingine.

download latest music    

Ben Pol alipokuwana akiojiwa na Jonijo,  wa onlinetv, alisema kuwa katika wasanii hawa wa kike wawili yaani wema Sepetu na Jokate Mwegelo hakuna hata mmoja ambae anaweza kutoka nae , lakini alipoulizwa sababu hakujibu nini kinamfanya asema kitu kama hicho.’Ikitokea natakiwa kutoka na Wema Sepetu au Jokate Mwegelo, sitatoka na mtu yoyote, ni bora nitoke mwenyewe’ huku akionekana kucheka, Ben Pol aliongea.Hata hivyo Ben Pol alisema kuwa mwanamke anaemtaka ni yule mwenye kujiamini hata wakiwa wanachart anakuwa anamuona huyo ni mwanamke anaejiamini

Tofauti kwa Ben pol, kunakuwa na wasanii kibao katika tasnia ya muziki waliowahi kutamka kutamani kuwa na mahusiano na wakinadada hawa wawili hasa Wema Sepetu, ilhali kila mwanaume ana sifa zake kwa mwanamke lakini wengi wanaonekana kuvutiwana warembo hawa waili huku kila mmoja akitoa sababu zake.

Tukiachana na historia ya kimuziki , Ben Pol ni baba wa mtoto mmoja wa kiume na kwa muda sasa umepita tangu kuwe na tetesi za yeye kuachana na mama wa mtoto wake ambae walikuwa wakiishi pamoja lakini taarifa hizo hazikuthibishwa na yeye mwenyewe , na baada ya hapo ndipo issue ya yeye(Ben Pol)  kutoka na Ebitoke ilipoanza kusambaa kwatika mitandao.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.