Ben Pol- Nilikuwa Chawa wa Barnaba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka na kukiri kuwa siku za nyuma alishawahi kuwa chawa wa msanii mwenzake Barnaba Boy Classic.

Ben Pol amewataka mashabiki kuacha kushangaa urafiki wake na Barnaba umeanzia wapi kwani ukifatilia historia ya muziki wake alishawahi kuwa chawa wa Barnaba.

download latest music    

Ben Pol amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv:

Kwanza watu wengi watakuwa hawafahamu urafiki wetu na Barnaba umeanza siku nyingi sana nilikuwa najiweka kwake kwa sababu nilikuwa naona anaimba vizuri na pia nakumbuka nilikuwa hata namsindikiza studio kwa Allan Mapigo.

Siku hizi hao watu wanawaita hao watu chawa kwaiyo mimi ndio nilikuwa chawa wake yaani namsindikiza lakini uchawa unasaidia hasa uchawa wenye malengo ambao hata mimi ni nao sahivi nina chawa wangu ambao wananifuata kila sehemu”.

Ben Pol amekiri kuwa kupitia kuwa chawa wa Barnaba alijifunza vitu vingi anavyojua leo hii kuhusu mziki kwaiyo uchawa wake ulikuwa wa faida.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.