Bifu Za Wasanii Zinazoendelea Bongo Zinaua Muziki

Kumekuwa na mifarakano mingi inayoendelea katika tasnia ya muziki tanzania, mara nyingine ugomvi unaokuwa unatokea unaweza kusababishwa na kitu kidogo tu ambacho inawezekana wasanii wenyewe wangekaa bila kufuata hisia za mashabiki wasimgefikia hatua ya kugombana kwa muda mrefu, wapo wanaogombana kwa sababu ya mambo binafsi yasiyohusiana na muziki.Kwa mwaka 2016-2017 zimezuka bifu nyingi na zingine zikiendelea kuongezea kadri siku zinavyozidi kwenda.Na hizi ni baadhi ya bifu za wasanii kwa mwaka 2016-2017.

1.Alikiba na Diamond Platinumz

download latest music    

Hakuna anaeweza kukujibu chanzo cha ugomvi wao ambao kila kukicha unachukua sura  mpya, ni ugomvi mkubwa ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kuumaliza wangeweza kukusanya mashabiki wengi kwa pamoja.

2.Diamond na Ommy dimpoz

Ni moja kati ya watu walikuwa na umoja sana walipoanza muziki, baade walikuja kutengana.Lakini bifu lilizidi kuw akubwa baada ya ommy kuungana na alikiba katika kazi hivyo Ommy akaanza kuwa upande wa Alikiba.bifu hili limeingiza hadi watu wa familia ya Diamond na inasemekana kuna kesi mahakamani kutokana na ugomvi wa wasanii hawa.

3.Young Dee,Young killer na Dogo Janja

Bifu lilianza kiutani utani lakini likazidi kukua, wasanii hao wanaona kuwa kila mmoja ni bora zaidi ya mwingine,kila mmoja hataki kufananishwa na mwingine, lakini kama wasanii wadogo wanaofanya vizuri katika sanaa walitakiwa kuungana ili kuendelea kuongeza idadi ya mashabiki.

4.Bob Junior na Diamond Platinumz

Kumekuwa tu na malalmiko ya upande wa Bob Junior kuhusu wawili hao kutokuwa na ushirikiano, ingawa anasema kuna mengi yanaendelea hapo katikati ikiwemo la wao kushindwa kukaa pamoja na kutatua tofauti zao kutokana na Diamond kutokuwa tayari, Diamond amekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu ili ingawa Bob Juniour ndie amekuwa akifunguka kila mara kuhusu Diamond.

5.Man Fongo na Sholo Mwamba

Bifu lilianza pale man fongo alipomtuhumu Sholo Mwamba kufiksha habari za umbea kuhusu Wema Sepetu, ni mambo flani binafsi ambayo yaliwezekana kutatuliwa kimya kimya.Singeli ni muziki unaoshikakwa kasi kwa sasa Tanzania hivyo wasanii hawa walipaswa kuwa ndugu ili kukuza muziki huu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.