Bill Nas Amefungukia Tuhuma Za Kupenda Kufanya Kolabo na Wasanii wa Kike Tu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bill Nas anayefanya vema kabisa kwa hivi sasa na wimbo wake wa ‘Tagi bovu’ amefunguka na kuongelea tuhuma zinazomkabili ya kwamba anafanya sana Kolabo na watoto wa kike kwa sababu ana Mahusiano nao.

Billnas amefanya Kolabo nyingi sana na wasanii wa kike kuliko hata kiume na kuna madai kuwa wasanii hao wa kike kuliko hata wa kiume na kuna madai kuwa wasanii hao wa kike aliofanya nao collaboration kuna ambao amekuwa nao kimapenzi.

download latest music    

Billnas ameshafanya kolabo na wasanii mbali mbali wa kike kama vile Rosa Ree, Dayna Nyange, Nandy, Linah na Mwanadada Nazizi kutoka Kenya na hivi karibuni ana Kolabo mpya na Mwasiti insyoitwa ‘Bado’.

Billnas amefungukia tuhuma hizo wenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews ya EATV ambapo amekataa tetesi hizo na kusema hazina ukweli wowote:

Habari hizo sio za kweli kabisa kwa sababu mimi nimefanya Kolabo na wasanii wengi wa kike Kasoro wachache tu lakini sina Mahusiano nao hawa wote ni dada zangu tu alafu isitoshe mimi sina dada kwenye familia yetu”.

Lakiji pia Billnas amesema aneshafanya kazi na wasanii wa kiume wengi tu kama Country Boy, Mwana FA, TID, Edu boy na amesema anategemea kupiga kazi na Ben Pol na Gnako.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.