Billnas Achoshwa na Skendo za Mapenzi Kila Siku Juu Yake

Msanii wa muziki bongo anaetamba na kibao chake kipya cha tag ubavu , Blnass amefunguka na kuongelea jinsi mitandao ya kijamii inavyokuwa inamharibia kazi na mahusiano yake kwa kumsambazia habari ambazo sio za kweli hasa katika swala la mahusiano.Bilnass anasema  kuwa hakuna kitu kinamkera na kumnyima amani  kama anapopata skendo hizo  za kuwa na mahusinao na wasanii wenzake kwa sababu vitu hivi sio vya kweli na vimekuwa vikimkosesha amani kabisa.

Bilnass anasema kuwa inamfanya anashindwa kufanya  kazi zake kwa sababu amekuwa akisingizia  kuwa na  mahusiano na watu ambao yeye yupo nae karibu kikazi tu na wala sio vinginevyo.Lakini pia skendo hizo mara nyingi zinamfanya anakosa amani katika mahusiano yake ya kweli kwa sababu mpenzi wake wakati mwingine anaamini kuwa ni kweli anatoka na wasanii wenzake.

download latest music    

sipendi sana pale ninapozushiwa kuwa natoka kimapenzi na waanii wenzangu kwa sababu niakosa amani na mahusiano yangu ya kweli.hizi skendo zinakuwa zinaniharibia sana kwa sababu hata yule niliyenae katika mahusiano kuna muda mwingine anahisi kuwa maneno hayo ni ya kweli kuwa nina mahusiano na watu waliotajwa ukiangalia nina ukaribu nao, hi inaniharibia sana.-Bilnass anatoa dukuduku lake alipokuwa akifanya mahojiano na  Ful shangwe ya GPL.

Katika mitandao, Billnass amewahi kuzungumziwa kuwa na mahusiano ya kimapezni na Dayna Nyange kutokana na ukaribu waliokuwa nao kipindi wanatoa wimbo wa Komela, ikaja tena akazushiwa kutoka kimapezni na Nandy na sasa hivi katika mitandao amepata skendo nyingine ya kutoka kimapenzi naip-hop mwana h Rosa ree kwa sababu ya kazi yao mpya iliyowafanya kuwa karibu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.