Billnass Atoa Sababu ya Kumpenda Sana Mama Yake.

Msanii wa bongo fleva Bilnass amefunguka na kutoa sababu ya kuwa siku zote amekuwa akimtaja sana mama yake kuliko baba yake na kwamba hata katika moja ya wimbo wake alionekana kumpondea  baba yake.

Billnas anasema kuwa amekuwa akifanya hivyo ili kuwapa moyo na motisha wamama wote na kujiona kuwa wao ni bora zaidi ili kufanya kazi vizuri kwa bidii.

download latest music    

Namsifia sana mama yangu ili kuwapa motisha wanawake wengine  na kuendelea kupambana  zaidi, sio kwamba baba yangu sio bora zaidi hapana lakini baba yangu ni mtu mzuri na amekuwa akinisaidia sana  na ni mtu mzuri na anaendelea kunisaidia tu  na yupo kwa ajili yangu kila siku na huwa siona kama kuna haja ya kumtaja baba kwa sababu inajulikana kuwa baba ni kichwa cha familia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.