Bilnass Kula Sahani Moja na Alikiba

Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya ‘Tagi Ubavu’ amefunguka na kuweka wazi kwa jamii kuwa Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambaye anampa ushirikiano mkubwa kwa kila jambo ambalo huwa analifanya katika harakati zake na kudai siku zikikaribia huenda wakatoa wimbo wa pamoja.

Billnass ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 jioni baada ya kuonekana picha katika mitandao za kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa studio katika siku za nyuma kidogo.

download latest music    

Nina mahusiano mazuri na Alikiba na huwa ananishauri mambo mengi katika kazi zangu hata muda mwingine huwa tunataniana, naamini anakubali kazi zangu maana huwa nikiachia ngoma huwa ananiambia mdogo wangu hapo fresh au kazia buti sehemu fulani. Inshallah panapo majaliwa nitafanyakazi na Alikiba ila kwa sasa sitaki kuliweka wazi suala hili, ila watu wajue tu kuwa tunamawasiliano mazuri baina yetu”, amesema Billnass.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.