Black Rhyno Ataja Sababu za Kupotea Kwenye Gemu

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyejikita katika miondoko ya kurap Nicholaus Haule maarufu kama Black Rhyno ambaye pia ni mdogo wa mkongwe wa Bongo fleva Joseph haule ‘Profesa jay’ ametaja sababu za yeye kutosikika Kwenye gemu kwa miaka kadhaa.

Black Rhyno alitamba miaka ya nyuma na wimbo wake wa ‘Black chata’ Uliompa umaarufu sana na hata kupata nominations kwenye tuzo kubwa za Africa za Channel O.

download latest music    

Black Rhyno alipotea kwenye gemu na akawa hasikiki kabisa. Hivi karibuni amerudi na ujio unaoitwa Panda Mnazi ambao video yake amefanya na Director Msafiri wa Kwetu Studio.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi, Black Rhyno amefunguka kutaja sababu ya yeye kupotea Kwenye gemu:

Sijapotea sana Nipo, lakini kwenye muziki sipo kimya kiivyo maana mara kwa mara nimekuwa nikitoa ngoma sema ndo’ vile hazifiki mbali.

Lakini pia ushindani  umeongezeka siyo kama zamani. Kwa sasa kila nyumba Dar, kuna msanii. Na wasanii wenyewe kila mmoja anakomaa kuhakikisha anafanya poa, kwa hiyo ushindani ni mkali.

Black Rhyino amewataka mashabiki zake waendelee kumpa sapoti kwa nyimbo yake mpya aliyoitoa inayoitwa Panda Mnazi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.