Bob Junior Aongelea Bifu Lake Na Q-Chillah,Blue Nae Atajwa

Bob junior amekuwa ni moja ya wasanii wanaoingia katika ugomvi mara nyingi tena hasa na wasanii ambao walianza chini ya lebel yake, miezi kadhaa iliyopita msanii huyu ambae pia na lebel yake, alisikika katika vyombo vya habari akizungumzia bifu lake na msanii Diamond Platinumz na kusemakuwa Diamond amekuwa akimkaushia kuwasiliana nae.

Akionge na eNews ta EATV, msanii Bob Junior ambae anafanya vizuri na kibao chake kipya kwa sasa  anasema kuwa watu wameanza kumzushia katika mitandao kuwa ana bifu zito na Q-Chillah lakini maneno hayo hayana ukweli wowote na aliamua kumuonyesha mwandishi mpaka meseji ambazo Q-Chillah amekuwa akimtumia kwa kumpongeza kuhusu kazi nzuri aliyoitoa hivi karibuni na kumpa ushauri , Bob Junior anasema”Q-Chifu ni kaka angu amenielekeza vitu vingi sana katika muziki, sina bifu na Q-Chifu,nina kazi zake nyingi binafsi, mi siwezi kugombana na Q-Chifu,kwa sababu nampenda ,ni kaka yetu wa muziki na ni baba yetu pia

download latest music    

Pia anasema kuwa watu wanozungumza katika mitandao kuwa Q-Chillah ameacha album shalobaro record kwa sababu ya bifu lao sio kweli na kwamba wamuache q-Chillah mwenyewe azungumze lakini sio wao.

Hata hivyo akizungumzia tetesi za kuwa yeye na .Mr.Blue wanakuwa na ugomvi kutokana na yeye kuwa anaimba kwa ku-rap kama Mr.Blue ,Bob Junior amefunguka na kusema kuwa yeye haimbi kwa kumuiga mtu yeyote , ila amekuwa akifanya kazi zake kama yeye na kwa sasa anataka kuwa na albumu mbili yaani album ya kuimba na ya kuchana lakini sio kwamba kuna mtu anamuiga.

mimi sichani kama mtu yeyote, mimi nachana kama mimi Bob Junior, mimi ninaimba sanaa,na kwanza ninampango wa kuwa na album mbili ya kuimba na album ya ku-rap, nataka niwafundishe marapper kuwa mimi ni rapper bora zaidi, mimi nina punchline hakunaga” aliongezea Bob Junior

Kuna kuwa na bifu zinazoanza chinichini kwa baina ya wasanii huku wakiwa hawana sababu ya msingi, wengine wakiingiza mambo yao binafsi katika kazi za musiki, hata kama wasanii wanakuwa wanaoneana wivu ,basi wivu huo uwapelekee kufanya muziki uendelee.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.