Bongo Kunamkondesha na Kumpausha Diamond;-Babu Tale

Meneja wa msanii mkubwa Afrika na Duniani kwa ujumla, Babu Tale amefunguka na kuongelea ya moyoni baada ya kusema kuwa amegundua kuwa kinachomfanya Diamond apauke na kukonda ni kwa sababu ya shida na matatizo anayokumbana nayo akiwa hapa bongo.

Babu Tale anasema Diamond amekuwa akifanya sana kazi kiasi kwamba kuna muda anakuwa akikesha kama msanii anaetoka  na ku-hustle ili kujulikana katika game wakati yeye ndio anapaswa kutulia na kula matunda yake kwa sasa.

download latest music    

Hata hivyo Babu Tale kupitiaukurasa wake wa instagram , anasema kuwa wameamua kumtengeneza na kumrudisha Diamond kupitia Universal ambapo hii itakuwa ni dili jipya kwa diamond kusaini.

nimegundua bongo kuna mpausha msanii wangu,videmu na madeni ya wasanii kusimamaia tv kama alishawahi kuwa nayo utotoni , kusakamwa na kukesha studio  utazani ametoka hivi juzi, kujitia udairekta  katika kazi za wasanii utazani alisomea tangu utotoni,nilichoamua ni kuongea na universal kijana abaki huko huko mpaka msimu wa wasafi festival .Mjue uwa unaniumiza sana mnapomsakama sana msanii wangu mpaka mnamfananisha na marehemu bi kidude…sasa nimamua arudi na nina imani Universla watanisaidia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.