“Bongo Movie Wengi Hatupendani Hasa Wanawake”- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa wasanii wengi wa Bongo movie wanachukiana na kusababisha tasnia hiyo kushuka kila siku.

Shamsa amepasua chuki walionayo wasanii wengi kwa Wenzao hasa wanawake inasababisha kukoseshana madili ambayo yangeweza kuitangaza nchi kwa ujumla.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo Movie Shamsa amefunguka haya zaidi:

Ni kweli kwa sababu Bongo Movie wengi hatupendani, hasa wanawake hatupendi kuwa mabalozi wazuri kwa wanawake wengine, kwa hiyo mwisho wa siku zile chuki zinafanya isiendelee.

Lets say mtu anatoka nje anataka kufanya kazi na Shamsa, unaanza kuponda usifanye naye kazi, mwisho wa siku dili linaondoka wakati ngingefanya ningewakilisha wasanii wa Bongo na pia Tanzania, so chuki inasababisha kushuka kwa Bongo Movie”.

Kwa muda mrefu wasanii mbali mbali wa Bongo movie wamekuwa wakinyosheana vidole kuhusu nini hasa kilichosababisha kuzorota kwa tasnia hiyo kuliko kutafuta njia mbadala za kuokoa tasnia hiyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.