Bongo Movies Tunapesa Msituchukulie Poa:-JB

Msanii mkongwe wa bongo movies Jacob Steven amefunguka na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwadharau sana wasanii wa maigizo na filamu kuwa hawana ela na ndio wanaoongoza kwa kuwa na njaa kwa sababu kazi zao zimekuwa hazifanyi vizuri na wamekuwa wakikosa masoko ya kazi zao.

Akiongea alipokuwa na wasaniii wenzake katika kampeni iliyozinguliwa jana na wasanii wengine wakiwepo huku kampeni hiyo ikiwa na lengo la kutafuta vipaji  na kuhamasisha vijana kujikita kufanya kazi hasa ya sanaa kwa sababu inalipa kuliko kukaa vijiweni na kujibweteka, anasema kuwa  kazi ya sanaa ina ela na hata wasanii wa bongo movie wana ela kwaio watu wasichukulie poa kazi hiyo.

download latest music    

Wasanii wa bongo movies wameamua kufanya kampeni hiyo ili kukuza kazi za sanaa za filamu kwa sababu kwa muda mrefu sasa kumekuwa na maneno kuwa  bongo movie imekufa j=na hata wasanii wake ni maskini.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.