Brown Aongelea Mahusiano Yake Na Wolper

Kulitokea tetesi nyingi hivi karibuni kuhusu mahusiano ya msanii wa bongo movies Jackline Wolper na mpenzi wake Brown ambae alifuta picha za Jacky zote baada ya kusemekana kuwa alichukizwa na kitendo cha Jacky kwenda katika birthday party ya Diamond Platinumz na kukutana na mpenz wake wa zamani Harmonize.

Akiongea na Friday Nite Live ya EATV, Brown ambae ni video model  anafunguka na kuongelea mahusiano yake na msanii huyo wa kike wa bongo movies na kusema kuwa Jacky ni mwanamke pekee ambae alishawahi kumpenda na bado ataendelea kumpenda daima na wala hana mpango wa kumuacha.Brown akisema kuwa Jacky ni mwanamke ambae amepitia mambo mengi tangu ameingia katika sanaa na tangu ameanza kuwa maarufu hivyo, maswala madogo madogo ambayo mpaka sasa yanaendelea katika mitandao na maneno anayozushiwa ni ya kawaida kwa sababu alishawahi kukutana na makubwa zaidi ya hayo.

download latest music    

Hata hivyo Brown alisema kuwa meseji zilizovuja hivi karibuni zikimuonyesha Jacky anachat na mpenzi mpya wa Harmonize sio za ukweli hata kidogo kwasababu hata yeye alipoangalia meseji zile alijua kuwa ile haikuwa charting ya mpenzi wake. ‘Zile meseji si zake, sio Jacky kabisa mimi najua mwandiko wa mwanamke wangu,yaani hata kama mtu akichukua simu ya Jacky akachart na mimi ninakuwa najua kabisa huyu sio Jacky’

Brown alifunguka na kusema kuwa kati ya wanawake kumi alikuwa nao tangu aanze mahusiano ,Jacky bado anampa namba moja na kutaja baadhi ya mambo ambayo yanamfanya amuweke Jacky katika nafasi iyo aliyataja pia kuwa ni “Nampenda sana Jacky nae ananipenda sana, kwanza ana heshima ni tofauti  na wanawake wengine ukimwambia kitu atakujibu weweeeee..,pili Jacky ni mcha mungu sana , familia yake ni ya dini na familia yangu ni ya dini pia.

Akiendelea kuongea, Brown alikana tetesi za watu kusema kuwa pamoja na kuwa Jacky yupo na yeye lakini yupo mwanaume mwingine mwenye fedha anaemuhudumia Jacky kifedha na kusema kuwa wao wamependana hivyo wanachojari ni mapenzi na wala sio kingine”kama alikuwa anafanya hivyo ni  kwa wanaume waliopita lakini sio kwangu maana ye mwenyewe anajua nini ninampa

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.