Calisah Amefunguka Kuhusu Mkwanja Mrefu Aliopata Baada ya Kuvaa Viatu Vya Kike

Mwanamitindo maarufu anayejulikana kama Calisah amefunguka na kudai kuwa kwa mwaka huu wa 2017 hakuna kazi iliyomuingizia kipato kikubwa kama kuvaa viatu vya kike.

Mwishoni mwa mwaka huu Calisah alizua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kurusha picha kwenye Instagram akiwa amevaa viatu vya kike jambo lililo washangaza watu wengi huku kila mmoja akitafsiri kitendo kile kivyake lakini mwenyewe alijitetea na kudai kuwa ilikuwa ni kazi to Kama kazi nyingine.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa redio kupitia kipindi Chao cha Planet Bongo Calisah amefunguka na kudai kuwa dili hilo alilipata kwa ajili ya kutangaza viatu vya kike Instagram kutoka kampuni Fulani na dili hilo lilimuingizia kiasi cha shilingi milioni saba za kitanzania.

Hili lilikuwa ni moja kati ya dili lililoniingizia hela ndefu kwa mwaka 2017 hadi mpaka hivi sasa ninavyoongea bado limevunja rekodi sijawahi kupata dili kama lile hata matangazo niliokuwa nayafanya tofauti tofauti kwa kipindi kile hayajafikia ile amount niliyolipwa kwa kuvaa vile viatu vya kike”.

Baada ya picha hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kila mtu aliongea lake na hata wapo waliodai kuwa Calisah atakuwa ni shoga kutokana na kuvaa viatu vya kike jambo alilokataa kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa yeye ni rijali na wala sio shoga.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.