Calisah Atangaza Kuja na Mikorogo Kwa Ajili Ya Wanawake

Mwanamitindo maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa Calisah Abdulhamid amezidi kushangaza wengi baada ya kutangaza kuja na mikorogo kwa ajili ya Wanawake.

Calisah ameweka wazi kuwa ana mpango wa kufungua duka  lake ambalo atajikita katika kuuza vidonge ambavyo vitatumika kutakatisha ngozi za Wanawake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Calisah ambaye amehusishwa mara kibao kubadili ngozi yake na kuwa mweupe, alisema weupe wake umetokana na AC za magari na si vinginevyo kama watu wanavyoeneza.

Hapana sijawahi badili rangi ya mwili wangu, mimi ndo nipo hivihivi tangu zamani, kubadili ngozi kwanza ni mambo ya kike ambayo sijawahi kufanya hivyo, hizi ni AC tu za magari halafu mimi ni mtu ambaye naamini sana kwenye muonekano wa kiume ndiyo mana hata nafanya mazoezi, kwa hiyo sijawahi kufanya hivyo kwa sababu hata familia yangu ni ya watu weupe.

Kwanza nipo mbioni kufungua duka la dawa za vidonge vya kung’arisha ngozi kwa wanawake ambapo Bongo hii hakuna, mimi ndiyo nimeagiza pekee na nitakuwa naziuza ofisini kwangu”.

Calisah amekuwa Kwenye headlines za Media mbali mbali tangu wiki iliyopita alipotangaza kufungua kampuni ya kuwapa Wanawake mimba.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.