Calisah Kushiriki Mashindano Ya Mr. Africa 2018

Model na mwanamitindo maarufu Bongo anayejuliakana kama Calisah amefunguka na kueleza Bahati ya mtende iliyomuangukia ya kwenda kushiriki mashindano ya Mr. Africa mwaka 2018.

Calisah amedondokewa na zali la kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya kushiriki Shindano la Mr Africa International, ambalo linachukua mtu mmoja toka Afrika na kumpeleka nchini humo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Calisah amesema kwamba imekuwa ni furaha kubwa sana kwake kualikwa kwenda nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mr Afrika, hivyo anaimani kubwa kuwa atafanya vizuri na Tanzania itakuwa namba moja na ndiyo maana sasa hivi anafanya sana mazoezi.

Nilitumiwa barua mwaka jana ya kwenda kushiriki Mr Africa International, lakini nilishindwa kwenda kwa sababu kwanza nilichelewa kupata barua yao halafu pia nilitakiwa kujilipia tiketi ya ndege mwenyewe kwenda na kujilipia hoteli kwa siku kadhaa ambazo ningekuwepo huko.

Lakini kwa bahati nzuri tena mwaka huu wamenitumia tena mwaliko, kwa hiyo natakiwa kwenda Nigeria mwezi wa 10 kwa ajili ya hayo mashindano na mimi ndiyo Mtanzania pekee ambaye nimechaguliwa kwenda na ninajua kabisa nitashinda”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.