Carol Ndosi Aandika Barua ya Wazi Kwa mh Makonda.

Mwanadada Carol ndosi aliyekuwa mwanzilishi na muendeshajiwa tamasha la nyama choma festival ameandika barua ya wazi kwa Mh Paul Makonda huku akielezea kilio chake na jinsi ambayo maswala ya uongozi na makatazoya matamsha yanavyoua vipaji vya wasanii na kazi za wajasiriamali tanzania.

Carol anaandika barua hiyo kufuatiwa pia kukatazwa kwa tamasha la fiest atanzania ambapo lilitakiwa kufanyika jijin dar wikiedi hii na kukatawa kwa madai kuwa maeneo ya leaders club ni karibu sana namaeneo ya watu ambao wamelalamika kuwa wamkeuwa wakichoshwa na kelele.

download latest music    

Carol anasemakuwa hata yeye mwaka uliopita alikatazwa kabisa kufanya tamsah hilo katika uwanja huo kwa madai hayo lakini baadae aliaona matamasha mengine yakiendelea kufanyika , hata hivyo Carol anasema kuwa swala hilo linapaswa kufikiriwa na viongozi kwa sababu mwisho wa siku wanaumia sana ni vijana ambao walikuwa wakitegemea matamasha hayo kwa ajili ya kujipatia vipato na pia kuendeleza maisha yao ya kila siku.

Carol anasema kuwa anaamini mh paul makond kama kiongozi anatakiwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatatu matatizo  kama haya ikiwa ni pamoja na kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya shughuli kama hizo hasa inapoonekana kuwa maeneo husika hakuna sifa hizo.

Akijaribu kujitetea, Carol anasema kuwa anaamini kuwa hana ugomvi na Mh Mkuu wa mkoa na hata kipindi cha sakata la uongzo wake na majina mengi na kashfa nyingi za Mh Makonda hakuwahi kutia neno katika sehemu yoyote hata mitandaoni lakini amekuwa akijiuliza kwani amekosa nini kwa mh mkuu wa mkoa.

Hata baada ya kusambaa kwa taarifa hizo katika mitandao ya kijamii na kuongelea maeneo mbalimbali, Mh paul makonda alimjibu Carol kuwa amesikiasikia kuwa kuna mtu ameandika barua ya wazi lakini yeye hana anuani katika mitandao ya kijamii hivyo kama ana shda basi aandike barua iende ofisini kwake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.