Casto Dickson Ataja Sababu Za Kuchora Tattoo Ya Tunda

Mtangazaji wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka na kutaja sababu zilizomsukuma mpaka kufikia uamuzi wa kuchora tattoo ya jina la Tunda mkononi mwake.

Siku ya jana Casto alianika tattoo yake mpya Kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuonyesha jinsi gani amekolea kwa mpenzi wake huyo mpaka kuamua kuchora Jina lake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Casto amefunguka na kudai alitumia dakika 10 kuamua achore tatoo hiyo na hawezi juta kwa kuwa ameutendea haki moyo wake.

Mimi nimechora ile tattoo kwa sababu kiukweli nampenda yule mwanamke na siko naye kwa ajili ya kumpitia Hapana ila tuna malengo na kila mtu amepunga atabadilika na tumeamua kufanya maisha.

Tunda ndio mwanamke pekee ambaye nimechora jina lake mwilini mwangu kwaiyo watu watambue kuwa ana maana sana kwangu alafu kuna wanaosema kuwa ni mapema sana kwa mimi kuchora Tattoo ninachotaka watu wajue ni kuwa tumekuwa pamoja kwa muda mrefu mapenzi yetu hayajaanza jana wala juzi”.

Lakini pia Casto amesisitiza kuwa hata kama wakiachana yeye na Tunda hawezi kufuta ile tattoo lakini amesema anajua kuwa hawawezi kuachana watakuwa wote milele.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.