Casto- Ni Maamuzi Ya Tunda Mwenyewe Kuchora Tatoo Ya Jina Langu

Mtangazaji wa Kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka na kuweka wazi kuwa kama Tunda ataamua kumchora na yeye Tatoo ya Jina lake mwili mwake ni uamuzi wake binafsi.

Suala hili limekuja siku chache baada ya Casto kuanika hadharani tattoo yake aliyochora Kwenye mkono wake yenye Jina la mpenzi wake Tunda.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Casto aliulizwa endapo ni zamu ya mpenzi wake Tunda na yeye kuchora Tatoo ya Jina lake Casto amesema hadi kufikia hatua hiyo kuna jambo la tofauti baina yao na iwapo Tunda atafanya hivyo watu wataona.

Utamuona akichora, kama akichora utamuona akichora, ana maamuzi yake, yeah!. Kwa sababu kuchora tattoo si pete sisi tumeanza hivi tuna sababu zetu.

Tuna maana yetu ambayo itakuja kuwa tofauti kabisa, for the first time in Africa tuseme, mtakuja kuona, yeah”.

Wawili hao waliozama Kwenye penzi zito Miezi michache iliyopita wameweka wazi kuwa wana mipango ya kufunga ndoa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.