Chege Chigunda aeleza kwa nini hana ‘hit song’

Chege Chigunda anaeendelea kufanya kufanya vizuri na muziki wake hivi karibuni alifunguka kueleza kwa nini bado hajatoa hit song kutoka kwa nyimbo zake za hivi karibuni.

download latest music    

Akizungumza na Times Fm katika kipindi cha Twenzetu, Chege alifunguka kutaja sababu kadhaa anazoamini kuwa ni chanzo cha yeye kutokuwa na ‘hit song’ tangu mwaka jana. Chege alisema;

“Unajua kuna mabadiliko ya muziki, ukiangali Marekani nako ni hivyo hivyo, ukiangalia Nigeria ni hivyo hivyo… zamani ulikuwa akisikia ngoma imetoka Fall in love inakuwa Fall in love dunia nzima umeona ukisikia Do Me, basi dunia nzima lakini sasa kilichotokea Nigeria ndicho kinatokea sasa sio kwamba watu hawapigi mziki mkali, kuna vita ya muziki inafanyika,”

Aliendelea kuongeza kuwa

” Zamani ilikuwa unaona singo moja inatoka kwa mwezi ya msanii mmoja au unakuta singo mbili zinatoka, lakini sasa kwa siku zinatoka karibu singo saba hiyo ndio sababu.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua