Chege na Mpenzi Wake Wamkaribisha Mtoto Wao

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Said Juma maarufu kwa jina la usanii kama Chege chigunda ametangaza rasmi ujio wa mtoto wake siku ya Jumapili tarehe 11 ambaye amempa jina la Jada.

Chege na mpenzi wake wa siku nyingi Zahra wamebarikiwa na mtoto wao wa kwanza wa kike. Chege alitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

download latest music    

Ni kweli siku ya jana majira ya saa kumi jioni mtoto wangu alizaliwa namshukuru sana Mungu kwa sababu mtoto ni Baraka mimi na mama yake tuna furaha sana”.

Mkali huyo anayetamba na ngoma yake ya Kaitaba aliyomshirikisha Saida karoli aliweka wazi mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa ana mpenzi wanaishi wote lakini kuhusu kufunga ndoa amekiri yeye atakuwa mtu wa mwisho kuoa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.