Chidi Benz Akana Tetesi Za Kuokoka Baada Ya Kuonekana Kanisani

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Rashidi Makwiro maarufu kama Chiddi Benz ameibuka na kukataa tetesi zilizoenea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameokoka.

Tetesi za Chidi Benz kuokoka zilishika kasi baada ya picha za msanii huyo kuonekana akiwa stejini Kwenye kanisa la kilokole akiwa na msanii wa nyimbo za Injili Bonny Mwaitege.

download latest music    

Chidi Benz amekana taarifa hizo na kudai kuwa yeye hajaenda kanisani kwa sababu ameokoka bali alienda pale kwa sababu ya mualiko aliopata kutokana na shughuli iliyokuwa inaendelea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na EATV, Chidi Benz alifunguka yafuatayo:

Nilialikwa pale kama mgeni rasmi, kulikuwa kuna wabunge, wajumbe wa serikali, lakini mimi nilialikwa nisingeweza kukataa, tena nikaona ni bahati ni siku yangu ya kuzaliwa, nikaona kwa nini nisende nikasikiliza nikaungana nao, mimi ni Rashid Abdala Makwilo, sijabadilisha“.

Kuokoka kwa Chidi Benz kulihushishwa na matumizi yake ya madawa ya kulevya kwani Chidi ni muumini wa dini ya kiislamu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.