Chin Bees Adai Anachukizwa na Wasanii Wapenda Kiki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na miondoko yake ya kuchana Musa Ramadhani maarufu kama Chin Bees amekiri kuwa anachukizwa sana na wasanii wanaopenda kiki.

Chin Bees ameongelea suala la kiki kumkera kwa sababu kwa sasa kuna baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wazuri katika kiki kuliko kazi zao yaani skendo zinateka kabisa kazi zao.

download latest music    

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Chin Bees amesema anashangaa kuona wasanii wenzake wakifanya kiki mitandaoni wakati muziki ni biashara ambayo inahitaji ubunifu tu ili uweze kufanya vizuri na mashabiki wafurahie muziki wako.

 Mimi nachukizwa kwa kweli, wasanii wapo kwenye biashara kwa hiyo ni bora ukafanya kazi kwa ubunifu kuliko kufikiri kiki ndio itakayokufanya ukauza nyimbo zako, unaweza ukatengeneza kiki na bado usifanye biashara ukawa umejishushia heshima tu“.

Wasanii wengi wanapenda kutengeneza skendo fulani ambayo itawafanya wapate kuongelewa sana Kwenye mitandao ya kijamii kabla hawajaachia kazi zao ili waweze kupata airtime kubwa pale wanapotoa kazi zao.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.