Christian Bella Akana Skendo Ya Kutumia Madawa Ya Kulevya Ayala Mwenye Ushahidi Apeleke

Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini Christian Bella amerudi tena Kwenye vichwa vya habari kwa mara nyingine tena huku tuhuma za kutumia madawa ya kulevya zikizidi kumuandama.

Bella aliingia kwenye listi ya wasanii wanaosemekana kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na tetesi hizi zilianza mapema mwaka huu baada ya kushindwa kufika kufanya shoo ya mkesha wa mwaka mpya.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda,  Christian Bella amekana tuhuma hizo na kusema yoyote ambaye ana ushaidi kuwa yeye anatumia madawa apeleke huo ushahidi:

Watu waendelee kunihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, hii ni kama mimba, wasubiri hadi nitakapoathirika na unga ndipo watapata majibu kama natumia ama la, kwa sasa siwezi kujibu ndiyo ama hapana.

Nikisema hapana au ndiyo hakuna mtu atakayeweza kuniamini, hakuna mtu anayejua na hakuna anayeweza kukubali hilo, watu wanaoniambia natumia madawa ya kulevya watoe vithibitisho, hawajui maisha ninayoishi.

Hakuna mtu anayejua aina ya maisha yangu ninayoishi, waendelee kuongea ni kawaida tu kama navuta ama sivuti Mungu ndiye anayejua, hivyo waache wazungumze mengi kuhusu mimi. Ninachoangalia ni maisha yangu yanaendaje na wala simfuatilii mtu”.

Christian Bella alipotakiwa kutoa ushauri kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya alidai  kuwa hawezi kutoa ushauri kwa watu kama watumie au wasitumie madawa kwa kuwa kila mtu ana maamuzi yake na maisha yake.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.