Christian Bella Ampa Shavu Diamond, Amtaja Micheal Jackson

Mwanamuziki anaefanya vizuri sasa hivi na kibao chake cha Pambe amefunguka na kumsifia msanii mwenzake diamond platinumz kwa hatua kubwa anazokuwa anapiga katika muziki gasa katika kuukuza muziki huo.bella anasema kuwa diamond amekuwa akifanya vitu vizuri na vkubwa ambavyo mara ya kwanza vilikuwa vikiwa vya kushangaza watu lakini kadri siku zinavyozidi kwenda vinaanza kuonekana ni vya kawaida tu,

Diamond namu-apprecite sana amekuwa akifanya vitu vikubwa na vizuri sana, anafanya vitu ambavyo sio vya kuhadithiwa pembeni ila kila mtu amekuwa akiona, kwa mimi leo hata mtu akinimbia Diamond ameimba wimbo na Michael Jackson sitashangaa aisee kwa sababu kashafanya kolabo nyingi na wasanii wa Afrika na sasa kaamua kuhamia Marekani. Aliongea Christian Bella.

Kwaio imeshaanza kuwa ni kawaida  kwa sababu keshathubutu kufanya vitu ambavyo mwanzoni watu tulikuwa tunashangaa  lakini leo tunaona kuwa ni kawaida tu  na kwa mtu kama yeye ambae ameshafika huko kushushwa ni kazi sana.

Bela ameamua kusema maneno hayo baada ya kuona jinsi msanii huyo ambavyo amekuwa akijitahidi kupenyeza kimataifa na wasanii wakubwa Duniani katika kufanya muziki wa Tanzania kujulikana nje ya nchi.Hivi karibuni Diamond amefanya nyimbo za kolabo na wasanii wakubwa kama Morgan Heritage na Rick Ross.

download latest music    

Ukiachana na kufanya kolabo nyingi nje lakini pia Diamond amekuwa ni msanii aliyejitoa sana ili kuwasaidia wasanii wengine kuweza kuendelea kimuziki kwa kuwatoa katika lebo ya ke ya WCB.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.