Christian Bella Apunguza Idadi Ya Shoo Kutokana na Hali Ngumu

Mwanamuziki anayefanya muziki wa Dansi nchini Christian Bella amefunguka kuhusu mipango ya kupunguza idadi ya shoo alizokuwa anafanya hapo awali kutokana na hali ngumu.

Bella ameweka wazi kuwa kutokana na ikawa na hali ngumu ya kimaisha hivi sasa wamepunguza idadi ya shoo walizokuwa wanafanya kutoka shoo nne mpaka tano na kufanya shoo moja tu.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Over Ze Weekend, Bella anayetamba na Ngoma ya Shuga alisema kuwa, atakuwa akifanya onesho kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ndani ya Kiwanja cha Mzalendo Pub Kijitonyama Jijini Dar.

Mashabiki wangu najua wengi mnapenda tufanye makamuziki mara kwa mara lakini kutokana na vyuma kukaza nawaomba tufanye kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ndani ya kiwanja hiki“.

Wasanii mbali mbali wanaofanya muziki tofauti na Bongo fleva kama vile muziki wa Dansi, singeli, taarabu na hata hip hop wamekuwa wakilalamika kukosa soko baada ya mashabiki wote kugeukia muziki wa Bongo fleva.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.