Chuchu Hans Awatahadharisha Wanaopiga Picha Za Utupu

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wasichana maarufu katika tasnia ya bongo fleva na bongo movies kupiga picha za utupu na kurusha katika mitandao ya kijamii,moja ya wasanii wa bongo movies aliyeanza muvi kwa muda mrefu na anasema kuwa picha za utupu hazikuwahi kumsaidia katika kutengeneza jina lake amefunguka na kuwaasa wale wadada waliopo katikia tasnia hii kuacha kupiga picha za uchi kwa sababu itafika sehemu watajuta kuwa wanapiga picha hizo.

Mwanadada Chuchu  Hans ambae amezaa na msanii mwenzie Ray Kigosi amesema kuwa wadada wengi wamezoea kupiga picha za uchi lakini kuna kipindi watakapotaka kutulia na kufanya maisha hata watu wa kuwaoa watakosa kwa sababu ya matendo yao ya nyuma yatakuwa yanawahabisha kabisa.

download latest music    

Ninawatahadharisha tu wasanii wenzangu hasa wa kike  waachane na hayo mambo jaman, wengine hata nguo hawavaa eti kisa wanataka kuwa na umaarufu.mwanamke ukiwa hivyo baadae sasa  ukija kushtuka unakuta kuwa umeshajiaribia kila kona , hata mwanaume wa kutulia nae unakosa kutokana na matendo yako ya nyuma.mimi nilipata umaarufu kutoka katika filamu ya roho sita wala sikufanya jitihada hizo za kupiga picha za utupu kufanikisha ndoto zako. -Alifunguka Chuchu Hans

Wasichana wengi katika tasnia ya sanaa wanaamini kuwa kuvaa nguo za nusu uchi na kupiga picha zinazoonyesha maungo yao ni njia bora ya kujipatia umaarufu kwa sababu ya kuwa wanaongelewa katika mitandao lakini ukwli ni kwamba wanakuwa wanaharibu sifa za mwanamke bora na pia kwa maadili yetu sio kitu cha kukikazia kukifanya.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.