Daxx Cruz Asema Kitendo Alichokifanya Calisah Ni Aibu

Mwanamitindo wa kimataifa anaefanya vizuri katika kazi zake kutoka Tanzania ambae anaishi  na kufanya kazi zake Afrika ya Kusini, Daxx Cruz amefunguka na kuongelea kitendo alichokifanya mwanamitindo mwenzake anaechipukia calisah na kusema kuwa ni cha aibu hata kama analipwa ela. mwanamitindo huyo amedai kuwa kitendo icho cha yeye kufanya kazi za kike ni kuiaibisha tasnia hiyo.

Calisah ambae wiki chache zilizopita alionekana kupata donge nono la kufanya kazi ya kupiga picha akifanya marangazo ya viatu vya kike ilhali yeye ni mwanaume , hata hivyo baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika mtandao baadhi ya watu walianza kumsema na kukashifu kitendo icho kuwa ni tabia mbaya .
hata hivyo calisah mwenyewe hakuonekana kujali baadhi ya maneno ya watu katika mitandao badala yake alisema kuwa yeye ana uwezo wa kufanya kazi zote ilimradi tu kazi iyo iweze kumlipa ela itakayo msaidia kumudu maisha yake.

download latest music    

Akizungumza kwenye bongo magazine, Daxx Cruz anasema kuwa hata yeye yupo katika tasnia hiyo ya modelling kwa muda mrefu lakini hawezi kufikia hatua ya kufanya kazi kama hizo kwa sababu ni kazi ya kike na wapo models wa kike na kwa mwanaume aliekamilika hawezi kufanya kitendo kama hicho ambacho hajawahi kuona kimetokea  Afrika.Kwa kuongezea Daxx Cruz amesema kuwa kitendo alichokifanya Calisah ni kitendo cha aibu

Daxx Cruz ni mmoja wa wanamitindo wanaofanya vizuri nje ya tanzania, akiwakilisha tanzania na ameweza kuitangaza vizuri tanzania.hata huivyo sio mara ya kwanza kwa Daxx Cruz kumuongelea Calisah, mara ya kwanza alishawahi kusikika akisemakuwa Calisah hafai kuwa model kabisa na wala hana sifa za kufanya kazi hiyo, endapo ataenda nje ya Tanzania hatopata soko la kufanya modelling kabisa.

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.