Daxxo Chali Afunguka Kuhusu Nini na Hytham

Producer kutoka studio ya MJ Record amefunguka na kuongelea kile kilichodaiwa kuwa wivu wa mapenzi ndio uliomfanya yeye ashindwe kuendelea kuwa-manage wasanii wawili wa kike yaani Nini na Haitham.Wiki iliyopita mtengenezaji huyo wa muziki alitamka rasmi kuwa kuanzia sasa yeye na wasanii hao hawatakuwa  wakifanya kazi pamoja  kama kuna mtu atakaekuwa anataka kuendelea nao basi yeye anamkaribisha.

Kadri taarifa hizo zilivyokuwa zikiendelea kusambaa ilikuja ikasemekana kuwa Daxxo Chali na wasichana hao walishindwa kufanya kazi pamoja kutokana na wivu wa mapenzi huku msanii Ney wa Mitego akihusishwa kwa kiasi kikubwa katika sakata hilo.

download latest music    

Hata hivyo alipokuwa akiongea na Clouds E ya Clouds Tv Daxxo Chali alimwambia Shadee kuwa ni kweli vitu hivyo vinahusishwa na mapenzi lakini sio wivu bali ni utovu wa nidhamu uliosababishwa na mapenzi.Hata hivyo Daxxo Chali anasema kuwa kulikuwa na makubaliano ya kimkataba ambayo wasanii hao wameshindwa kuyafuata kwa kipindi cha muda mrefu hivyo kama yeye ameshindwa kuendelea kufanya nao kazi.

“Mkataba huwa ni confudentila lakini kwa kifupi walikosea katika kipengele cha nidhamu ambapo yakaja na maswala ya mapenzi , na mimi sikuwakataza wao kuwa na mahusiano kwa sababu hata mimi nina mahusinao yangu lakini inategmea na hayo mahusiano unayawekaje na inabidi yasiingiliane na kazi au kuharibu CV ya studio au producer”

Hata hivyo Daxxo Chali anasema kuwa wasichana hao walizidi kiasi kwamba alikuwa akipata taarifa kuwa leo wako na fulani na kesho na fulani na kesho kutwa na mwingine kitu kinachoharibu sifa ya msanii na msiamizi wake pia.Akendelea kufunguka kuhusu maneno aliyoyasema Ney wa Mitego kuwa Mj Records ina mambo ya kitoto kutokana na kushindwa kuendelea kuwasimamia wasanii hao, daxxo chali anasema kuwa “Ney ni mtu mzima lakini alikuwa akidate na mtoto, kwaio unaweza ukaona mtu huyo anaongea hivyo akili zake zikoje,na alichokiongea Ney mimi nimemuelewa yeye amejaribu kujitetea kwa sababu alikuwa anahusuika na hii issue kwa sababu alikuwa akitembea na Nini.”

Daxxo Chali  anasema kuwa hana wivu na wasanii hao kwa sababu alishakaa nao kabla ya kufanya muziki kwa zaidi ya miaka mitano sasa, na hawezi kuendelea kuwa nao kwa sbabu alishajaribu kukaa na wazazi wa wasanii hao zaidi ya mara nne kwa upande wa Haitham lakini hakuwahi kujirekebisha.

wasanii Nini na Haitham wanaosemekana kuwa na utovu wa nidhamu na kushindwa kuendelea kufanya kazi na Daxo Chali

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.