Diamond Aahidi Kubadilisha Maisha ya Wasanii.

Mwana muziki Diamond Platinumzamefunguka na kuwahakikishia wasanii wote watakao pata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha la Wasafi Festival linaloaanza mwaka huu kwamba atawapa ela nzuri na kwamba atajitahidi kuyainua maisha yao kupitia hilo.

Diamond ameyasema hayo alipokuwa akizindua chaneli ya wasafi tv katika kingamuzi cha star time  jijini dar june 19 mwaka huu na kupata fursa ya kuongea na waandishi wa habari.

download latest music    

Diamond anasema kuwa tamasha hilo halina haja ya kuua au kushindana na matamasha mengine yoyote yaliyowahi kuanzishwa huko nyuma,lakini lina lengo la kuinua wasanii na kutoa burudani.

Tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka lakini nitakuwa nina hakikisha kila msimu unapoisha wasanii wanakwenda nje ya nchi au wanaanzisha mradi kutokana na kile wanachokipata.

Tunaomba makampuni yajitahidi kujitokeza ili kutusapoti vijana ili kutia chachu katika tamasha hili liwe na manufaa kwa vijana wanapopata malipo .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.